Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa. 38
Mtume swala na salamu zimuendee amesema: aliadhibiwa mwanamke kwa sababu ya paka, alimfungia mpaka akafa, akaingia motoni, hakuwa anamlisha wala kumpa maji isipokuwa alimfungia,wala hakumuacha ale majani ya ardhi.( Mttafaqun alayhi)
Mtume swala na salamu zimuendee amesema:Mtu mmoja alimuona mbwa akila mchanga kwa kuingia,akachukua kiatu chake akawa anampa maji mpaka akatosheka, Allah akamshuhudia ,akamuingiza peponi.Amepokea Muslim na bukhari