Makubaliano ya wayahudi na wakristo, Uislamu katika kuweka ukali katika adhabu ya kosa la zinaa: Angano la kale:( Walawi: 20:10-18)
Katika ukristo,Yesu ameweka ukali katika maana ya uzinzi,wala hajafupisha katika tendo bali akaenda mpaka katika kuvuta picha kimaana. Ukristo umeharamisha wazinifu kutorithi ufalme wa mbinguni na hawana lingine zaidi ya adhabu ya milele ndani ya jahannam. Adhabu ya mzinifu katika haya maisha ni ile iliyotajwa katika sheria ya Musa kuwa auawe kwa kupigwa mawe. Agano jipya: (Matayo:5:30_27),(Wakorintho:(6:9-10) Yohana:8:3-11.
Kama wanavyokubali wasomi wakileo wa vitabu takatifu kubwa kisa cha Yesu kumsamehe mzinifu hakipo katika chapa ya injili ya Yohana ya mwanzo lakini baadaye ili waliokuja kuongeza. Muhimu ni kuwa Yesu alikwisha kutangaza mwanzoni mwanzoni mwa kulingania yake kubwa hakuja kuipinga alichokuwa nacho malaika wa Musa na manabii wengine kabla wake. Kuondoka kwa mbingu na ardhi ni bora kuliko kuondoa nukta moja katika sheria ya Musa. Kama ilivyo kuja katika Injili (Bible) Luka:16:17.(Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati)
Itasimamishwa adhabu baada ya kutolewa ushahidi na watu wanne pamoja na kuelezea tukio la zinaa lilivyokuwa hilo litatia nguvu kutokea kwake, moja ya hizo hoja ikiwa na nguvu adhabu itatolewa. Hii huonesha uchache wa kutolewa adhabu katika sheria za uislamu katika historia kwa sababu zinaa haitothibitika isipokuwa kwa njia hii na hili jambo la ushahidi ni gumu, hukaribia kutowezekana.
Katika hali ya kutolewa adhabu ya zinaa kwa upande mmoja kukiri bila mashahidi wanne basi hakuna adhabu kwa upande wa pili ambao haujakiri kosa.
Allah amjaalia mlango wa toba uko wazi.
Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima. 17
Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu. 110
Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu. 28
Uislamu unakiri mwanadamu kuhitaji maumbile. Lakini uislamu unafanya kazi ya kutimiza kulinda maumbile haya kwa njia ya kisheria: njia ya kuoa, inahimiza kuoa mapema, na inasaidia katika kutimiza hilo kwa kutumia mali ya umma(Baitul maal) ikitokea sababu zitakazo sababisha isitimie.,na inafanya pupa vile vile kusafisha jamii na njia zote za kueneza zinaa, kwa kuweka malengo makubwa ambayo yatatimiza uwezo na utekelezaji wake katika njia ya heri, pamoja na kushughulika wakati wa faragha na kuwa karibu na Allah. Hayo yote yanazuia kila lenye kupelekea kutendeka uovu wa zinaa. Pamoja na hayo uislamu hufanyi haraka kutoa adhabu ya zinaa mpaka uthibitisho wa tendo la zinaa upatikane kupitia mashahidi wanne. Pia ijulikane pia kuwa kuwepo kwa mashahidi wanne inapunguza kutokea kwa adhabu ,isipokua kwa hali ambayo mtendaji wa kosa kakiri mwenyewe hapo atakuwa anastahiki adhabu kali. Jambo la zinaa ni katika madhambi makubwa sawa sawa iwe wazi au kisiri.
Alikuha mwanamke mmoja kwa Mtume swala na salamu zimuendee akikiri na kutii kwake (pasina kulazimishwa) akamtaka apewe adhabu,na alikuwa na ujauzito wa zinaa. Mtume akamuita akamwambia msimamizi(walii) wake : mtunze vizuri. Na hii inatonesha ukamilifu wa sheria ya kiislamu na ukamilifu wa huruma za Muumbaji kwa viumbe.
Mtume akamwambia rudi mpaka ujifungue. Wakati aliporudi Mtume akamwambia: nenda mpaka umwachishe ziwa mwanao, alirudi baadaye tena baada ya kumuachisha ziwa ndipo akamuadhibu. Akasema ametubia toba ambayo laiti ingegawanywa kwa watu sabini wa mji wa Madina ingewatosha.
Huruma ya Mtume Swala na salamu zimuendee imeonekana katika tukio hili tukufu.