Uislamu umetukuza vipi mwanamke?

Uislamu imemtukuza mwanamke umemsamehe kutokana na makosa ya Nabii Adamu kama ilivyo katika itikadi zingine, uislamu umefanya haraka katika kunyanyua hadhi ya mwanamke.

Katika uislamu Allah amemsamehe Adamu na ametufundisha vipi turejee kwake tukikosea katika maisha. Allah amesema:

Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. 37

Bibi Maryam mama yake Isa (Yesu) amani iwe juu yake ni mwanamke wa kipekee ambaye ametajwa kwa jina katika Qur-an mwanamke amechukua nafasi kubwa katika visa vingi ambavyo vimetajwa katika Qur-an. Mfano,Balqis malkia wa Sabai kisa chake na Nabii Suleiman hitimisho lake ni kuamini na kujisalimisha kwake kwa mlezi wa ulimwengu. Kama ilivyokuja katika Qur-an.

Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa. 23

Historia ya kiislamu imetuwekea wazi kuwa Mtume Muhammad alitaka ushauri kutoka kwa wanawake na akachukua wazo lako katika matukio mengi. Kama alivyowaruhusu wanawake kwenda msikitini kama wanaume kwa sharti wawe na haya na utulivu licha ya swala zao majumbani ni bora zaidi. Mwanamke alikuwa akishirikiana na wanaume katika vita katika kutoa misaada wa matibabu. Kama walivyokuwa wakishiriki katika miamala ya kibiashara na wakishindana katika kutoa elimu na maarifa.

Uislamu umefanya vizuri katika kumweka mwanamke katika nafasi yake ukilinganisha na tamaduni za zamani za waarabu uislamu ukawakataza kuwazika watoto wakike ikampa mwanamke utu kamili, pia uislamu umepangilia mambo yanayohusu ndoa pale ulipochunga haki ya mwanamke katika mahari.Ukadhamini haki yake ya mirathi na haki yake ya kumiliki mali yeye mwenyewe..

Mtume swala na salamu zimuendee amesema: Muislamu aliyekamilika imani ni yule mwenye tabia nzuri sana, na mtu bora kwenu ni yule aliyebora kwa wake zake. (Amepokea At-tirmidhy)

Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa. 35

Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.

Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.

Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. 97

Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao

Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri. 21

Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua. 127 Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. 128

Allah amewaamrisha wanaume kuwapa matunzo wanawake na kuhifadhi mali zao pasina ya mwanamke kuwa na usimamizi wowote wa mali katika familia kama uislamu ulivyohifadhi utu wa mwanamke pale ukipomruhusu kuhifadhi jina la familia yake baada ya kuolewa.

PDF