Mwanamke kabla ya uislamu alinyimwa mirathi, wakati uislamu ulipokuja ukamjumuisha katika mirathi bali yeye anaweza kupata fungu kubwa kuliko wanaume au wakagawana sawa kwa sawa. Mwanamke baadhi ya wakati atarithi na mwanaume asirithi Wanaume hupata fungu kubwa kuliko wanawake kulingana na ukaribu walionao na marehemu na fungu katika hali nyingine , ndiyo hali inayoelezwa katika Quran tukufu:
Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili..."[210]. (AN-NISAAI 11)
Bibi mmoja muislamu siku moja alisema hakuwa akielewa jambo mpaka alipofariki baba mkwe wake, mumewe alirithishwa mara mbili ya kile alichorithi dada yake(wifi yake), mumewe akanunu kupitia urithi huo vitu ambavyo hakuwa navyo kama vile nyumba ya familia yake na gari. Dada naye akanunua johari/vito pesa nyingine akaziweka benki, huku mumewe ndiyo mwenye jukumu kuhakikisha wanapata makazi na mahitaji mengine ya muhimu. Sasa hivi akafahamu hekima ilipo nyumba ya hii hukumu. Akasema Alhamdulillah.
Hata kama katika jamii nyingi mwanamke anafanya kazi kwa ajili ya kuendesha familia hukumu ya wanamke katika hili haiondoki. Mfano simu imeharibika kwa sababu mtumiaji ameshindwa kufuata masharti ya matumizi ya simu ,sio hoja ya kuwa hayo masharti kutofaa.