Muislamu anafuata mfano wa watu wema na masahaba wa Mtume, anawapenda na anajaribu kuwa wema kama wao, na anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake kama walivyofanya, lakini hawatakasi wala kuwafanya kuwa mpatanishi baina yake na Mwenyezi Mungu.
"... wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu..."[168]. (Al Imran: 64).