Aya ya kwanza:"Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu...." [154] Kanuni kuu ya Kiislamu iliamuliwa, ambayo ni katazo la kulazimishwa katika dini. Wakati aya ya pili ""Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho..."(155)Mada yake ni makhsusi, inayohusiana na wale wanaozuilia njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaowazuia wengine kuukubali wito wa Uislamu, kwa hiyo hakuna mgongano wa kweli baina ya Aya hizo mbili. (Al-Baqarah: 256). (Al-Tawbah: 29).