Nini thamani ya maisha ya duniani?

Mtihani huwekwa ili kutofautisha wanafunzi kwa viwango na madaraja wanapoanza maisha mapya ya kazi. Licha ya kuwa mtihani ni mfupi, huamua hatima ya mwanafunzi kuelekea maisha mapya anayokabiliana nayo. Vivyo hivyo, maisha ya duniani, licha ya kuwa mafupi, ni kama nyumba ya majaribu na mtihani kwa wanadamu, ili waweze kutofautishwa kwa viwango na madaraja wanapoingia kwenye maisha ya Akhera. Mwanadamu huondoka duniani akiwa na matendo yake na siyo na mali za dunia. Kwa hivyo, mwanadamu anapaswa kuelewa na kutambua kwamba anapaswa kufanya kazi katika dunia kwa ajili ya maisha ya Akhera na kutafuta malipo ya Akhera.

PDF