Wakristo, Wayahudi, na Waislamu katika Mashariki ya Kati hutumia neno 'Allah' kumaanisha Mungu, ambalo linamaanisha Mungu mmoja wa kweli, Mungu wa Musa na Yesu. Muumba mwenyewe amejitambulisha katika Qur'an Tukufu kwa jina 'Allah' na majina mengine na sifa. Neno 'Allah' limetajwa mara 89 katika toleo la zamani la Agano la Kale.
Na miongoni mwa sifa za Allah Aliyetukuka zilizotajwa katika Qur'an ni: Muumba.
"Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni Mwenye kushinda, Mwenye hikima" [Al-hashr : 24]
Yeye ni wa Kwanza ambaye hakuna kitu kabla Yake na wa Mwisho ambaye hakuna kitu baada Yake "Yeye ndiye wa Mwanzo na ndiye wa Mwisho, naye ndiye wa Dhaahiri na wa Siri, naye ndiye Mjuzi wa kila kitu" [Al-hadid: 3]
Mpangaji Msimamizi: "Anapanga mambo kutoka mbinguni hadi ardhini .." [As-sajda :5 ]
Mwenye elimu Mwenye nguvu :... " Hakika Yeye ni Mwenye elimu Mwenye Nguvu " [Fatir-44]
Hajidhihirishi katika sura ya yeyote kati ya viumbe Vyake : ... " Hakuna kifano chake . Naye ni mwenye kusikia mwenye kuona" [Ash-shura : 11]
Hana mshirika wala hana mwana : "1 - Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. 2 - Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. 3 - Hakuzaa wala hakuzaliwa. 4 - Wala hana anaye fanana naye hata mmoja" [ Al-ikhlas 1-4 ]
Mwenye hikima : ... " Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye elimu Mwenye hikima " [ An-nisaa : 111]
Mwenye uadilifu : ... " Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote" [Al-kahf: 49]