Mungu wa kweli ni Muumba, na kuabudu miungu isiyokuwa Mungu wa kweli kunajumuisha madai kuwa wao ni miungu, na Mungu lazima awe Muumba. Ushahidi kwamba yeye ni Muumba huwa kwa kuona viumbe vyake vilivyomo ulimwenguni, au kupitia ufunuo "wahye" kutoka kwa Mungu ambaye imethebitishwa kuwa ni Muumba. Basi ikiwa madai haya hayana ushahidi, laa kutokana na uumbaji ulimwenguni unaoshuhudiwa, wala kutokana na maneno ya Mungu Muumba, basi hao miungu lazima wawe wa uongo.
Tunaona kuwa katika nyakati za shida, binadamu humwelekea ukweli mmoja na kumwomba Mungu mmoja tu. Na sayansi imeuthibitisha umoja wa materi na umoja wa mfumo katika ulimwengu kupitia kutambua maonyesho ya ulimwengu na matukio yake, na kupitia kufanana na kulingana katika kuwepo
Basi tufikirie kuhusu familia moja wakati baba na mama wanapokhitilafiana kuhusu kuchukua uamuzi wa dharura unaohusu familia, na matokeo ya tofauti zao ni watoto kupotea na kuharibika kwa mustakabali wao, je, itakuwaje kama kuna miungu miwili au zaidi inayoongoza ulimwengu?
Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema :
"Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua" [Al-anbiya - 22]
Pia tunakuta kuwa :
Inapaswa kuwa uwepo wa Muumba ulitangulia uwepo wa wakati, mahali, na nishati. Kulingana na hilo, asili haiwezi kuwa ndiyo chanzo kilichosababisha kuumbwa kwa ulimwengu, kwa sababu asili yenyewe inaundwa na wakati, mahali, na nishati, kwa hivyo sababu hiyo lazima iwe ilikuwepo kabla ya uwepo wa asili.
Inapaswa kuwa Muumba awe Mwenye nguvu, yaani awe na mamlaka juu ya kila kitu
Inapaswa kuwa uamuzi uwe mikononi mwake, ili atoe amri yake ya kuanza kuumba
Inapaswa awe na elimu kamili kuhusu kila jambo, yaani awe na maarifa kamili ya vitu vyote.
Inapaswa awe mmoja na wa pekee, hafai kuwa na haja ya kuwepo na chanzo kingine pamoja naye, wala hafai kuhitaji kujidhihirisha katika sura ya yeyote katika viumbe vyake, wala hana haja ya kuwa na mke au mtoto katika hali yoyote, kwa sababu anapaswa kuwa na sifa zote za ukamilifu.
Inapaswa awe Mwenye hekima, hafanyi kitu chochote isipokuwa kwa hekima maalum.
Inapaswa awe Mwadilifu, na katika uadilifu wake ni kutoa malipo na adhabu, na anapaswa kuwa na uhusiano na wanadamu, kwani hatakuwa Mungu kama aliwaumba na kuwaacha. Kwa hivyo, anatuma Mitume kwao ili kuwaelekeza njia sahihi na kuwafikishia wanadamu mafundisho yake. Basi yule anayestahili malipo ni yule anayefuata njia hii, na adhabu ni kwa yule anayeipotosha.