Njia ya amani ni nini?

Hitimisho la mwisho wa safari ya maisha na kuwasili kwenye fukwe za amani lipo katika aya hii:

Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. 69 Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyo yafanya, na Yeye anayajua sana wanayo yatenda. 70 Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri. 71Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi nayo ni ubaya ulioje wa makaazi ya wanao takabari! 72Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo milango yake imekwisha funguliwa. Walinzi wake watawaambia: Salaam Alaikum, Amani iwe juu yenu! Mmet'ahirika. Basi ingieni humu mkae milele. 73Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na akaturithisha ardhi, tunakaa katika Bustani popote tupendapo. Basi ni malipo mazuri yaliyoje ya watendao!.[331]. (Zumar :69-74)

NASHUHUDIA KUWA HAKUNA MOLA APASAYE KUABUDIWA KWA HAKI ISIPOKUWA ALLAH PEKE YAKE HANA MSHIRIKA.

NASHUHUDIA KUWA MUHAMMAD NI MJA WAKE NA NI MTUME WAKE.

NASHUHUDIA KUWA MTUME WA ALLAH NI WA KWELI.

NASHUHUDIA KUWA PEPO NI KWELI NA MOTO NI KWELI.

PDF