NI yapi mafikio ya yule ambaye hajafikiwa na ujumbe wa kiislamu.?

Hao kamwe Allah hatowadhulumu lakini atakuja kuwapa mtihani siku ya kiama.

Wanaadamu ambao walipata bahati ya kuuona uislamu vizuri hawa hawana udhuru. Kwa sababu kama tulivyotaja hawatakiwi kufupisha katika kutafuta na kufikiria. Licha ya kusimamisha hoja na kuisimamia ni ngumu kuhakikisha kutokana na hilo watu wanatofautiana.Udhuru wa ujinga au kutofikiwa na hoja jambo ni la Allah akhera. Upande wa hukumu za dunia zitaegemezwa katika uwazi.

Hukumu ya Allah ya kuawaadhibu sio dhuluma baada ya hija hizi zote alizozisimamisha kwao kama akili,maumbile,ujumbe,ishara za dunia na katika nafsi zao. Jambo ambalo walipaswa kufanya kutokana na yale waliyofaradhishwa juu yao ni kufanya mbadala wa hayo yote ni kumtambua Allah na kumpwekesha pamoja na kushikamana na nguzo za uislamu.Laiti wangefanya hivyo wangefaulu na kutodumu milele motoni. Waka kuhakikisha furaha duniani na akhera.Je unaimani hili ni gumu?

Hakika haki ya Allah kwa waja wake aliyowaumba ni kumuabudu peke yake, na haki ya waja kwa Allah ni kutomuadhibu yule ambaye hajamshirikisha yeye na chochote. Jambo ni jepesi, nayo ni maneno anayoyatamka mwanadamu na akayaamini na akayafanyia kazi kwa makusudio yake na yanatosha kumuokoa na moto. Je huu sio uadilifu?.Hii ndiyo hukumu ya Allah na ndiyo hukumu ya uadilifu ya Mpole na Mwingi wa habari.Hii ndiyo dini ya Allah aliyetukuka aliyejuu.

Tatizo la kweli halipo katika kukosea kwa mwanadamu au akifanya dhambi juu ya dhambi kwa sababu miongoni mwa tabia ya mwanadamu ni kukosea.Kila binadamu anakosea na aliyebora katika wakosaji ni wale wanaotumia.Kama alivyoeleza hivyo Mtume. Lakini tatizo lipo kuendelea kufanya madhambi na aibu pia ni mwanadamu kunasihiwa na asisikie nasaha na asiifanyie kazi, na akumbushwe na asinufaike na ukumbusho ,apewe mawaidha na asinufaike na mawaidha na asizingatie wala asitubie na asiombe msamaha bali anaendelea akiwa na kiburi..

Na (mtu kama huyo) anapo somewa Aya zetu huzipa mgongo kwa kujivuna, kama kwamba hakuzisikia, kama kwamba masikioni mwake mna uziwi. Basi mbashirie kuwa atapata adhabu chungu."[330].( Luqmaan:7)

PDF