Miongoni mwao haki ya mwanadamu ni kutafuta elimu na kuitafuta katika pembe za dunia hii. Allah ametupa sisi hizi akili tuzitumie na sio kuziharibu. Wanadamu wote wanafuata dini za baba zao pasina kutumia akili na pasi na kufikiria wala kuchambua dini hii. Hili bila shaka huku ni kuidhulumu nafsi. Kuidharau hii neema kubwa ambayo Allah ametupa ambayo ni akili.
Waislamu wangapi wamelelewa katika familia ya tawhid (kiisilamu) wakatoka kwenye uislamu kwa sababu ya kumshirikisha Allah. Wapo wengine wamelelewa kwenye familia ya kishirikina au kikristo wanaamini utatu mtakatifu, wakakanusha imani hiyo wakasema: LAA ILAAHA ILLA LLAAHU( hakuna muabudiwa anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Allah).
Simulizi hii inaweka wazi jambo hili,pale aliposimama mke kupika samaki kwa ajili ya mumewe lakini aliondoa kichwa na mkia kabla kumpika huyo samaki . Ndipo mumewe akamuuliza: kwanini umekata kichwa na mkia?. Akasema (mke) mama yangu huwa anapika hivi. Mume akamuuliza Mama: kwa nini huwa unakata mkia na kichwa wakati ukitaka kupika samaki? .Mama akajibu: Mama yangu huwa anapika namna hii. Baada ya kumuuliza mama akamuuliza bibi: Kwa nini huwa unakata kichwa na mkia?. Bibi akajibu:Sufuria yangu ya kupikia ilikuwa ndogo ikanilazimu nikate kichwa na mkia ili niweze kumweka samaki kwenye sufuria. .
Ukweli ni kwamba matukio mengi yaliyopita na yaliyopita zama zilizopita zinafungamana na zama hizo, na zinasababu yake ambazo zinafungamana nazo, huenda simulizi hi iliyopita inaakisi hayo. Na ukweli ni kuwa hayo ni majanga ya kibinadamu kuishi katika zama ambazo sio za kwetu na tuige matendo yawenzetu bila ya kufikiria au kuuliza licha ya hali ni tofauti na kubadilika kwa zama.
Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao. [329]. (Ar-raad:11)