Allah amewaelekeza waja wake wote njia ya uokovu, wala haridhii ukafiri kwao, lakini yeye hapendi mwenendo mbaya wa ambao wanadamu hupitia wa ukafiri na uharibifu katika ardhi.
Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani. "[316]. (Az-zumar:7)
Tunasemaje kwa baba ambaye arudiarudia mbele ya wanawe kusema mimi ni najitapa kwenu nyote mkiiba,mkizini,mkiua na mkifanya uharibifu katika ardhi nyinyi kwangu mimi ni kama mfanya ibada mwema?. Bila kuficha sifa ya karibu zaidi ya huyu baba huyu ni kama shetani, anahamasisha uharibifu katika ardhi.