Kwa nini Allah anarudiarudia kutahadharisha na moto, Je hilo halipingani na sifa yake kiungu ya huruma?

Mama huwafunika wanawe kwa wingi wa kuwaonya kila wanaposafiri au wakielekea kazini kuwa wawe na tahadhari wakati wakiondoka na wakirudi.Je atazingatiwa kuwa ni mama mbaya?. Huku ni kugeuza mizani kuona kuifanya huruma ni ususuavu. Allah ana wazindua waja wake na kupitia huruma yake anawatahadharisha na kuwaongoza kuelekea njia ya uokovu, akaahidi kubadili maovu yao kubwa mema endapo watakapotubia kwake.

Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [314]. (Alfurqan:70)

Kwanini uoni wetu hujageukia ukubwa wa thawabu na neema ya pepo za milele mbadala wa uchache wa utiifu?

Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu yake, na atamuingiza katika Mabustani yenye kupitiwa kati yake na mito, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa. [315].(At-taghaabun:9)

PDF