Allan ni mwenye huruma mno na yeye ndiye chimbuko la heri zote, kwanini hatotuingiza sote peponi bila kutuhesabu?

Kwa hakika, Mwenyezi Mungu anataka imani kwa waja wake wote.

lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani. 7

Pamoja na hayo atakapowaingiza wote peponi bila ya kuwahesabu itatokea ukelele wa uadilifu, Allah atawafanyia Nabii wake Musa na Firauni vile vile, na atamuingiza kila mwenye kudhulumu na kuchinjwa chake peponi kama vile hakuna kitu kilitokea. Kuna haja ya namna ya kuhakikisha wale ambao wanaingia peponi wanaingia kwa kuzingatia misingi ya sifa.

Hakika uzuri wa ufundishaji wa uislamu ni kuwa Allah anafuhamu kuliko sisi tunavyojifahamu wenyewe. Allah ametujulisha kuwa ni lazima tuchukue sababu za kidunia kwa lengo la kupata radhi zake na kuingia peponi.

Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho.

PDF