Ni ipi hekima ya Muumba kuumba Majanga ya asili?

Allah ameweka kanuni za asili na mienendo za kuhukumu, nazo hujilinda wakati wakutokea uharibifu au matatizo ya mazingira na hulinda ili kuwepo uwiano kwa lengo la kutengeneza dunia na kuhakikishamaisha yanaendelea katika namna bora. Mambo yanayowanufaisha watu na maisha ndiyo yanayodumu katika ardhi, na wakati yakitokea majanga katika ardhi wanadamu wanadhurika mfano maradhi,volkano, matetemeko ya ardhi na mafuriko ndipo majina na sifa za Allah zinaonekana kama Mwenye nguvu, Mwenye kuponya, Mwenye kuhifadhi, katika uponyaji wa mgonjwa na kumhifadhi aliyeokoka au huonekana jina lake la Mwenye uadilifu katika kumuadhibu mwenye kudhulumu mwenzake na mkosaji,na huonekana jina lake la Mwenye hekima katika kutahini na kuwapa matatizo asiye kubwa muovu, atamlipa kwa wema yule atakaye subiri na adhabu kwa asiye na subira. Katika hili atafahamu mwanadamu ukubwa wa Mola wake kupitia mitihani hii pia uzuri wake katika utoaji wake. Asipofahamu mwanadamu isipokuwa tu sifa ya uzuri ya kiungu basi ni kama bado hajafahamu Allah mshindi na mtukufu.

Kuwepo kwa majanga,shari na maumivu ilikuwa ni sababu ya kukufuru wengi katika wanafalsafa wa sasa kama vile "Antony Flew" kabla ya kifo chake alikiri kuwa Allah yupo licha ya kuwa kiongozi wa upinzani katika nusu ya pili ya karne ya ishirini.Alikiri uwepo wa Mungu(Allah):

"Hakika kuwepo kwa shari na maumivu katika maisha halipingani na uwepo Mungu (Allah) lakini yeye anatusukuma kujua sifa za kiungu." "Antony Flew" anaona kuwa hayo majanga yana faida, zina amsha uwezo wa mwanadamu kwa hiyo anafanya haraka yanayoleta amani kama yanayoamsha uwezo wa kimwili inayopelekea kuwasaidia watu. Uwepo wa shari na maumivu umepelekea maendeleo ya ustaarabu wa binadamu katika historia. Akasema:hata hoja ziwe nyingi za kufafanua hili jambo ufafanuzi wa kidini ndio utakubali sana na ndio unaendana na uhalisia wa maisha. (Nukuu kutoka : "Khurāfat al-Ilhād" by Dr. ‘Amr Sharīf, chapa ya mwaka, 2014 BC.

Uhalisia unaonesha kubwa sisi wakati miwingine tunawashika mikono watoto wetu wadogo kwa mapenzi yote tunawaingiza chumba cha upasuaji ili wapasuliwe matumbo yao na sisi tunaimani moja kwa moja kwa hekima ya tabibu/daktari kwa mapenzi yake kwa mtoto kuwa atafaulu kumpasua salama.

PDF