Je shari unatoka kwa Allah?

Shari haitoki kwa Allah. Shari sio katika mambo yaliyokuwepo. kilichopo ni heri tupo.

Mfano mtu akampiga mwingine mpaka akashindwa kutikisika,atakuwa amechuma sifa ya dhuluma. Na dhuluma ni shari.

Lakini kuwepo kwa nguvu kwa yule anayechukua fimbo na ampige nayo mwingine sio shari.

Kuwepo kwa matashi aliyopewa na Allah sio shari.

Kuwepo na uwezo wa kutikisa mkono hii sio shari.

Kuwepo na sifa ya kupiga kwa fimbo sio shari.

Mambo yote yaliyopo kwa yenyewe tu ni heri.Wala hayawezi kuwa na sifa ya shari mpaka yalete madhara kwa kutumia vibaya.nayo ni maradhi ya kupoza kama ilivyo katika mfano wa kwanza.Mfano kuwepo kwa nge ya nyoka sio shari yenyewe ila akijitokeza ila mpaka apate kwa binadamu. Allah mtukufu hanasibishwi na shari katika matendo yake ambayo yana heri tupu. Katika matukio ambayo ameyaruhusu yatokee kwa hukumu yake na mipango(kadari) yake ni kwa hekima maalum na ndani yake kuna maslahi ya vitu vingi pamoja na uwezo wake wa kuzuia yasitokee, matokeo yake mwanadamu kutumia heri hivi kimakosa.

PDF