Katika Quran kuna aya nyingi ambazo zinaonesha huruma ya Allah n'a mapenzi yake kwa waja wake, lakini mapenzi ya Allah kwa waja wake hayafanani na mapenzi ya waja wake wenyewe kwa wenyewe. Kwa sababu katika vipimo vya kibinadamu ni haja ndiyo humfanya amtafute mpenzi wake, atapata haja yake kwa mpenzi wake.Lakini Allah ni mkwasi kwetu, mapenzi yake kwetu ni mapenzi ya fadhila na huruma, mapenzi ya mwenye nguvu kwa dhaifu na tajiri kwa masikini, mwenye uwezo kwa asiye na uwezo, mkubwa kwa mdogo mapenzi hayo ni ya hekima.
Je tuwaruhusu watoto wetu wafanye kila wanachokitaka kwa hoja ya kuwa tunawapenda? .Je tuwaruhusu watoto wetu wadogo wajitupe dirishani au kwenye nyanja za umeme zizochunika kwa hoja ya kuwapenda?
Haiwezekani maamuzi ya mtu mmoja yeye maslahi na manufaaa binafsi au kumfanya yeye ndio kituo muhimu na iwe kufikia malengo yake binafsi ndio kipaumbele zaidi kuliko kuzingatia mji na athari za jamii na dini, na imruhusu kubadili jinsia yake na afanye atakalo,avae na afanye njiani atakalo kwa hoja hii njia ya umma.
Lau mtu ataishi na kundi la watu katika nyumba moja kwa kushirikiana, Je atakubali mmoja wao ajisaidie haja kubwa au ndogo sebuleni kwa hoja ya hiyo ni nyumba ya wote? Je atakubali kuishi katika hii nyumba bila masharti yoyote.? Mwanadamu akiwa na uhuru wa moja kwa moja atakuwa mbaya, kama ilivyothibiti bila shaka hawezi kuvumilia huu uhuru.
Nadharia ya Ubinafsi chombo kamili mbadala wa umma mzima hata nguvu ya mmoja mmoja iweje au mamlaka yake. Mtu mmoja mmoja katika jamii ni matabaka hawezi kuwa katika hali nzuri ila kwa kumtegemea mwingine.Hatosheki mpaka kwa mwingine.Wapo wanajeshi, matabibu, wauguzi, mahakimu, vipi yeyote kati yao aridhie anufaike na apate maslahi yake binafsi kutoka kwa mwingine atimize furaha yake, na awe yeye ni chanzo kikuu umuhimu?
Kumuachilia moja kwa moja mwanadamu ndio itakuwa tabia yake hivyo milele, Allah anamtaka awe ni kiongozi wake,Allah anamtaka mwanadamu mwenye akili, hekima anayehukumu tabia yake. Haitakiwi kwake kuzembea katika tabia badi aiongoze ili itawale roho na aitathimini nafsi.
Pale ambapo inampasa baba kwa watoto wake kuwapangia baada ya muda wa kufanya marudio ya masomo,ili wafikie malengo yao ya masomo hapo usoni, pamoja na kutamani kwao kucheza tu, Je kwa hili huyu baba ataonekana ana roho ngumu?