Vifo vilivyotokea wakati wa Hijja haijatokea ila kwa miaka kadha tu. Lililozoeleka ni kuwa wanaofariki kwa sababu ya msongamano ni wachache. Lakini mfano wanaofariki kwa sababu ya pombe ni wengi mamilioni kila mwaka, mkusanyiko katika viwanja vya mipira ya miguu na sikukuu ya Kanivali huko Marekani ya kusini na zaidi ya hayo.kwa hali yoyote mauti ni kweli na kukutana na Allah ni kweli , mauti katika kumtii Allah ni bora kuliko mauti katika kumuasi Allah.
Malcolm X anasema:
"Kwa mara ya kwanza baada kuishi ya miaka 29 juu ya ardhi nilisimama mbele ya muumba wa kila kitu nikajihisi mimi ni mwanadamu aliyekamilika, sijapatapo kushuhudia katika maisha yangu kitu cha kweli mno zaidi ya udugu kati ya watu kutokana rangi zote na utaifa, Marekani inahitaji kuufahamu uislamu kwa sababu ndio dini pekee inayomiliki njia ya kutatua matatizo ya ubaguzi wa rangi." Mlinganizi wa kiislamu anapigania haki za binadamu Marekani mwenye asili ya Afrika (Mmarekani mweusi) amesahihisha muelekeo wa harakati za kiislamu Marekani baada ya hizo harakati kuachana kwa nguvu na aqida(imani) ya kiislamu na akalingania aqida sahihi.