Je kwa mfano tutamtia aibu mtu anayebusu bahasha ambayo ndani yake kuna barua kutoka kwa baba yake?. Ibada zote za hijja ni kusimamisha kutajwa kwa Allah. Na kujulisha kumtii na kujinyenyekeza kwa mola wa ulimwengu wala haikusudiwa ni ibada ya kuabudu mawe au kuabudu sehemu au mtu. Uislamu unalingania katika ibada ya muabudiwa mmoja naye Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao naye ni muumba wa kila kitu na ni mmiliki wake.
Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina. (Al-anaam:79)