Kuna tofauti kubwa kati ya dini za waabudu masanamu na kutukuza sehemu na ibada fulani sawa sawa iwe ya kidini au kitaifa au kijamii.
Mfano kurusha vijiwe(jamarat) kulingana na baadhi ya kauli ni kwa ajili ya kuonesha sisi kupingana na shetani na kutomfuata na kuiga vitendo vya bwana yetu Ibrahim juu yake amani pale shetani alipotokea ili amzuie kutekeleza amri ya Mola wake ya kumchinja mwanawe akaanza kumrushia mawe.Hivyo hivyo kukimbia kati ya Swafa na Marwa pia ni kuiga matendo ya bibi Hajar pale alipofanya juhudi ya kutafuta maji kwa ajili ya mwanaye Ismail. Katika hali zote na baadhi ya mitazamo katika maoni hususani hili, Ibada zote za hijja ni kusimamisha kutajwa kwa Allah. Na kujulisha kumtii na kujinyenyekeza kwa mola wa ulimwengu wala haikusudiwa ni ibada ya kuabudu mawe au kuabudu sehemu au mtu. Uislamu unalingania katika ibada ya muabudiwa mmoja naye Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yao naye ni muumba wa kila kitu na ni mmiliki wake. Imamu Al-hakim katika Almustadrak na Imamu Ibnu Khuzayma katika Sahih yake kutoka kwa Ibni Abbas Allah (amemridhia na aendelee kumridhia).