Kwa nini uelekeo wa kibla cha swala ulibadilishwa kutoka Masjid Aqswaa kwenda Masjid Haram wa Makka?

Alkaaba imetajwa sana katika historia na watu huitembelea kila mwaka kutoka sehemu za mbali na nchi za kiarabu na wanaheshimu utukufu wake mataifa yote ya kiarabu. Katika Angano la kale pia Alkaaba imetajwa. "Wakipita kati ya bonde la Bakkah, Hulifanya kuwa chemchemi..."[300]

Waarabu walikuwa wanafunika nyumba tukufu kabla ya kutumwa Mtume.Baada ya mtume Muhammad swala na salamu zimuendee kutumwa mwanzoni kabla ya utume Allah alifanya Baitul Maqdis kuwa ndiyo kibla chake, kisha akamuamrisha abadilishe kibla aelekee nyumba tukufu ( Batul Haram Makkah) mpaka wajulikane wafuasi wa kweli wa Muhammad na watakatifu kwa Allah na wajulikane wale waliokataa. Lengo la kubadilishwa kibla ni kuzitakasa nyoyo kwa ajili ya Allah na kuziepusha na kumtegemea mwingine, mpaka wakajisalimisha waislamu wakaelekea kibla walichoelekezwa na Mtume. Mayahudi walilifanya jambo Mtume kuswali kuelekea Baitul Maqdis kuwa ni hoja yao ya kujitetea.(Agano la Kale:Zaburi:84)..

Pia kugeuzwa kwa kibla ili kuwa ni mwanzo wa mabadiliko na ishara ya kuondoka uongozi wa kidini kwenda kwa Waarabu baada ya kunyang'anywa Waisraeli na hilo ni kutokana na wao kuvunja ahadi za Mola wa Ulimwengu.

PDF