Allah ameifanya Alkaba kuwa ni nyumba tukufu , nyumba ya kwanza ya ibada na nembo ya umoja wa waumini, pale ambapo wanaelekea waislamu wote wakiswali kutoka katika sehemu tofauti ya ardhi kituo chao ni Makka. Qur'an inatueleza matukio mengi katika vitendo vya wafanya ibada pamoja na mazingira yanayowazunguka kama tasbihi, kusoma kwa milima na ndege pamoja na nabii Daudi. "Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, (tukasema): Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia. Na tukamlainishia chuma" (suratul Sabaa:10.)
Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote [299].(Al-imraan:96) Alkaaba tukufu ni jengo la pembe nne inakaribia kuwa umbo la mraba , ipo katikati msikiti mtukufu wa Makka tukufu. Jengo hili lina mlango lakini halina madirisha. Ndani yake hakuna chochote na sio kaburi la yeyote. Ni chumba cha kuswalia. Mtu ambaye ataswali ndani ya Alkaaba ataswali kuelekea upande wowote. Alkaaba imerudiwa kujengwa mara nyingi katika historia. Nabii Ibrahim ndiyo alirejea kunyanyua upya nguzo za nyumba akishirikiana na mwanaye Ismail. Katika nguzo ya Alkaaba kuna jiwe jeusi na inaaminiwa ilikuwepo tangu zama za Nabii Adamu.Lakini hili jiwe halina maajabu yoyote au miujiza ni jiwe linaloashiria nembo ya waislamu.
Mzunguko wa asili wa dunia husababisha usiku na mchana na kujumuika waislamu kuizunguka Alkaaba na kuswali kwao swala tano kwa siku kutoka sehemu mbalimbali ya dunia na kuelekea kwao Alkaaba huwakilishwa mfumo wa ulimwengu katika mawasiliano ya kudumu yenye kuendelea katika kumtukuza,kumsifu/kumtakasa mola wa ulimwengu. Hii ni amri kutoka kwa Mola aliyemuumba Nabii Ibrahim kunyanyua nguzo za Alkaaba na kuizunguka pembezoni mwake na akatuamrisha Alkaaba iwe ni uelekeo/kibla cha swala.