Kwa nini muislamu anaswali mara tano kwa siku?

Muislamu anafuata mafundisho ya Mtume Muhammad Swala na salamu zimuendee na huswali kama alivyoswali Mtume kwa ukamilifu.

Amesema Mtume swala na salamu zimuendee:" swalini kama mlivyoniona nikiswali" (294) (amepokea Al-bukhary)

Muislamu akiswali humsemesha mola wake mara tano kwa siku kwa mapenzi yake makubwa ya kuwasiliana na mola wake kwa siku. Na ndio kiunganishi ambacho Allah ametuwekea ili tuongee naye na akatuamrisha tulazimiane nayo kwa maslahi yetu.

SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda. [295]. (AL - A'NKABUT: 45)

Sisi binadamu tunawasiliana na wake/waume zetu na watoto wetu kwa simu kila siku, hili ni kutokana na mapenzi yetu makubwa kwako.

Umuhimu wa swala unaonekana pale inapoikataza nafsi na kufanya maasi na huisukuma nafsi kufanya heri na hilo hupatikani pale anapo jielekeza kwa muumba wake na kuogopa adhabu yake na akitarajia msamaha wake na thawabu zake.

Kama ilivyo matendo ya mwanadamu hapana budi yawe ni kwa ajili ya Mola wa ulimwengu peke yake na pale ambapo ni ngumu kwa binadamu kukumbuka kwa muda mrefu au kuleta nia upya ikawa hakuna budi kuwepo na nyakati za swala kwa ajili ya kuwasiliana na mola na kufanya upya kumtakasia yeye ibada na matendo naye ni nyakati tano usiku na mchana ambazo zinaakisi nyakati na mambo makuu ya wazi kwa kugeuka usiku na mchana katika ya siku.( Alfajiri, adhuhuri,al-asri, Magharibi na ishaa).

Yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla halijachwa, na nyakati za usiku pia umtakase, na ncha za mchana ili upate ya kukuridhisha. [296]. (T'AHA: 130).

Kabla ya kuchomoza na kabla ya kuzama kwa jua.: Swala ya Alfajiri na Al-asiri.

Nyakati za usiku: swala ya ishaa.

Na ncha za mchana: swala ya Adhuhuri na Magharibi.

Swala tano ina funika mabadiliko ya mazingira ambayo yanatokea katikati ya siku kwa kumkumbuka muumba wake na mvumbuaji wake.

PDF