Kwa nini muislamu anaswali?

Muislamu anaswali kwa mtii mola wake aliemuamrisha kuswali, ameifanya hiyo swala ni nguzo katika nguzo za uislamu.

Muislamu anasimama kuswali kila siku saa kumi na moja asubuhi, huku marafiki zake wasio kuwa waislamu wanafanya mazoezi ya viungo muda huohuo wa asubuhi. Swala kwake ni chakula cha mwili na roho, na mazoezi kwao ni chakula cha mwili pekee yake. Wakati dua ni kuomba Allah kwa haja haihitaji mtikisiko wa mwili kama kuinama kusujudu , muislamu hulifanya hilo wakati wowote.

Tuangalie namna tunavyojali miili yetu huku tukiacha roho zetu zikipata tabu matokeo yake ni kutokea kwa matukio ya kujiua yasio hesabika yanayofanywa na watu wanaoishi katika maisha ya starehe hapa duniani.

Swala inapelekea kuondoa hisia zilizopo katika ubongo , hasahasa hisia binafsi na hisia za wanaotuzunguka, hili humpelekea mwanadamu uwezo mkubwa katika kuwa na raha. Kuhisi hivi hawezi kuelewa yeyote ila yule aliyejaribu hilo.

Vitendo vya ibada husisimua kituo cha hisia katika ubongo na ugeuka itikadi kutoka katika nadharia mpaka inakuwa ni uzoefu wenyewe. Je baba atatosheka kumkaribisha mwanaye aliyetoka safarini kwa mdomo? . Akili haitotulia mpaka amkumbatie na ambusu. Kila mwenye akili ana matakwa ya kimaumbile katika kuipata itikadi na fikra umbile la kihisia, zikaja ibada kuzitumia matakwa haya. Kuabudu na utiifu hujipa umbile katika swala ,funga n.k

Dkt. Andrew Newberg (293) anasema: "Ibada ina nafasi kubwa katika kuimarisha afya ya mwili,akili na roho pia kuleta utulivu na raha ya roho. Hivyo hivyo kuelekea kwa muumba huzidisha utulivu na raha". (Kiongozi katika Kituo cha masomo ya kiroho katika Chuo cha Pennsylvania Marekani.)

PDF