Shahada na kukiri upweke wa muumbaji na kumwabudu yeye pekee yake, na kukiri kuwa Muhammad ni mja wake na ni mtume wake.
Kudumu kuwasiliana na mlezi ulimwengu kwa njia ya swala.
Kutia nguvu matashi ya mwanadamu na kuhukumu mwenyewe na kukuza hisia za huruma na kuwa kitu kimoja na wengine wakati wa funga.
Kutoa fungu dogo katika anachomiliki kuwapa mafakiri na masikini kwa njia ya zaka, zaka nayo ni ibada inayomsaidia mwanadamu kuwa na sifa ya kujitoa na kutoa na kuepukana na ubakhili na uchoyo.
Mumbaji(Allah) kutenga wakati na sehemu maalum ya kutekeleza ibada ya hija na matendo ya hijja ni waislamu wote kwa kwenda Makka. Hiyo ni nembo ya umoja wa waumini wote, katika kuwaongoza licha ya utofauti wao kimataifa ,kitamaduni , kilugha, hadhi na rangi.