Kwa nini uislamu imekatazwa kunywa pombe.?

Allah amemtofautisha mtu na mnyama kwa akili.Allah ametukataza lile linalotudhuru na linalodhuru akili na miili yetu kwa hiyo ametukataza kila chenye kulewesha ,kwa sababu kina funika akili na kinaizuru na kinapelekea uharibifu. Mfano mlevi kumuua mwenzake au kuzini au kuiba na kadhalika katika uharibifu mkubwa unaotokana na kunywa pombe.

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa. [288]. (AL - MAIDA: 90)

Pombe ni kila chenye kulewesha bila kutizama muonekano wake na jina lake. Amesema Mtume wa Allah: Kila chenye kulewesha ni pombe,na kila chenye kulewesha ni haramu.( Amepokea Muslim) [289]

Uharamu wake ni kutokana na madhara yake kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Pombe pia imekatazwa kwa Wakristo na Wayahudi, lakini wengi wao hawalifanyii kazi hilo.

"Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima".[290] (Methali:20:1)

Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;[291] (Waraka wa Waefeso: 5:18)

Jarida maarufu kama "The Lancet" mwaka 2010 limechapisha tafiti ya madawa za kulevya yenye kuharibu jamii. Utafiti imeegemea katika aina 20 za madawa katika ya hayo mfano vinywaji ya Alkoholi , Heroine na Tobacco n.k. Tathmini ilifanyika kuangalia aina 16 na kati ya tisa zilimletea madhara kwa mnywaji mwenyewe na aina saba kwa wengine. Na tathimini ilikuwa zaidi ya asilimia mia moja.

Matokeo yalikuwa tukichukulia kwa kuzingatia madhara ya mtu mmoja mmoja na kwa wengine yote kwa pamoja hakika pombe ndio kilevi chenye madhara zaidi na inachukua nafasi ya kwanza.

Na utafiti mwingine umeonesha matumizi salama ya pombe kuwa:

sifuri! ndiyo matumizi salama ya alcohol kuepukana na hasara ya kupoteza maisha kwa magonjwa na ajali ,yote yanasababishwa na unywaji huo wa pombe.Hivi ndivyo walivyokiri watafiti katika ripoti iliochapishwa katika tovuti ya jarida la dunia maarufu hilo hilo la "Lancet". Hii ndiyo tafiti iliyojumuisha uchambuzi mkubwa wa data kwenye mada hii mpaka sasa. Imejumuisha watu milioni 28 duniani wakitoka katika nchi 195 kati mwaka 1990 mpaka mwaka 2016 kwa kuzingatia ueneaji wa matumizi ya pombe na kiwango cha matumizi.( kwa kutumia vyanzo 694 vya taarifa maalum) na namna matumizi hayo yalivyoleta madhara ya kiafya kwa sababu ya pombe iliyotolewa na tafiti 592 zilifanyika kabla na baada ya ugonjwa.. Matokeo yanaonyesha kubwa alcohol ilisababisha vifo vya watu milioni 2.8 duniani.

Kutokana na maelezo hayo watafiti wametoa nasaha kuwa pombe ianzwe kutozwa kodi ilikuweka mipaka ya uwepo wake sokoni na kuenea. Hii ni kama hatua ya awali kuizuia sokoni hapo baadae. Amesema kweli Allah mitukufu pale aliposema :

Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? [292]. (AT-TIN: 8).

PDF