Maana ya mali katika uislamu ni biashara na kubadilishana bidhaa na wahudumu na katika kujenga na kuimarisha , na pale ambapo tutatumia mali kwa lengo la kuchuma sisi tutakuwa tumetumia mali katika lengo lake liilokusudiwa ,kama njia ya kubadilishana na kuongezeka na tutakuwa tumefikia lengo.
Faida au riba ambayo ni lazima katika mkopo huzingatiwa ni kinga kwa wakopeshwaji hivyo haiiangalii hasara. Upande mwingine faida ya kimahesabu ambayo hupata mkopeshaji baada ya miaka kupita itaongezeka ghafla kwa matajiri na mafukara. Katika miongo ya hivi karibuni mataifa na taasisi yamepata hasara kubwa.Tumeshuhudia mifano mingi ya kuanguka baadhi ya dola kiuchumi. Riba inauwezo wa kusambaza uharibifu katika jamii kwa sura isiowezekana na jambo lingine ovu kufanya hivyo. (282)
Allah amesema: Kwa kujibu wa sheria za kikristo Thomas Aquinas amelaani riba au mkopo wenye riba. Kanisa limeweza kwa maono mapana ya kidini na kidunia kuharamisha riba kwa wafuasi wake baada ya kuharamisha kwa makasisii wake tangu karne ya pili. Kwa mujibu wa Thomas Aquinas sababu zilizopelekea kuharamishwa ni kuwa faida haiwezi kuwa thamani ya kumkopeshaji kumsubiri mkopaji kwa sababu wanaona wafanyakazi ni katika biashara.Hapo mwanzo mwanafalsafa Aristoto ana amini kuwa mali ni njia tu ya biashara na sio njia ya kupata maslahi, kwa upande wa Plato alikuwa anaona katika riba kuna ukandamizaji hutumiwa na matajiri kuwakandamiza masikini katika jamii.Miamala ya riba ilikuwa mingi katika zama za Wagiriki. Ikawa ni haki ya mdai kumuuza mdaiwa sokoni la watumwa endapo akishindwa kumlipa deni lake. Waroma wao walikuwa hivyo kuharamishwa huku haikuwa kutokana na msukumo wa kidini kwa sababu lilitokea kabla ya kuja ukristo kwa zaidi ya karne tatu, tambua pia Biblia ilikwisha haramisha kwa wafuasi wake na piaTorati.
Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.[283]. (AL I'MRAN: 130).
Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye. [284]. (AR-RUM: 39).
Angano la kalenga limeharamisha riba pia , ukiangalia mfano katika Walawi sio kwa ufupi:
"Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri. Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe..Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.[285].(Wakati:25:35-37)
Kama tulivyotaja mwanzoni kubwa sheria ya Musa Ndio sheria ya Bwana Yesu kwa kuwa inaafikiana na yale yaliopo katika Agano jipya kwa ulimi wa Yesu.
17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.[286](Matayo:5:17-19)
Kwa kusisitiza hilo riba ni haramu kwa wakristo na kwa wayahudi vilevile.
kama imekuja katika qurani tukufu
Basi kwa dhulma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyo halalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu. 160 Na kuchukua kwao riba, nao wamekatazwa, na kula kwao mali ya watu kwa dhulma. Basi tumewaandalia makafiri katika wao adhabu yenye uchungu. [287]. (AN-NISAAI: 160-161).