Hakika miongoni mwa huruma za Allah na upole wake ni kuturuhusu kula vizuri na kutukataza kubwa vichafu.
Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.[277]. (AL I'MRAN: 157)
Wanasema baadhi ya walioingia katika uislamu kuwa nyama ya nguruwe ndio sababu ya wao kusilimu.
Hapo mwanzo walikuwa wanajua kuwa huyu mnyama ni mchafu mno na anasabisha magonjwa ya mwili , wakachukia kula mnyama huyo.Kwa hakika waliamini kuwa waislamu hawali nyama ya nguruwe sio tu kwa sababu imeharamishwa katika kitabu chao kwa kuwatakasa na huyo mnyama mpaka walipokuja kujua kuwa kula nyama ya nguruwe ni haramu kwa waisilamu kwa sababu ni mnyama mchafu na nyama yake inadhuru afya, na kisha wakajua wakati huo ukutukufu wa dini hii.
Allah (aliyetukuka hali yakuwa yupo juu) anasema:
Yeye amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilicho tajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini aliye fikiwa na dharura bila ya kutamani wala kupita kiasi, yeye hana dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [278]. (AL-BAQARA: 173).
Na tutaonesha uharamu wa kula nyama ya nguruwe katika ngano la kale.
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.(279) (Wakati:8-7:11)
na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.(280) (Kumbukumbu la Torati:8:14)
Kama inavyofahamika kwamba sheria ya Musa ndiyo sheria ya Bwana Yesu pia yanaendana na yale yalipo katika Ngano jipya kwa ulimi wa Bwana Masihi.
17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.(281) ( Matayo 5:17-19)
Kwa hoja hiyo inazingatiwa kuwa nyama ya nguruwe ni haramu kwa wakristo vile vile pia kwa wayahudi.