Kuna tofauti kubwa kati ya roho ya mnyama na roho ya mwanadamu. Roho ya mnyama ni ile nguvu ya kutikisa mwili, roho ikitengana na mwili kwa kifo anakuwa mzoga usio sogea, hiyo ni aina ya uhai na mimea na miti nayo ina aina ya uhai pia wala haitoitwa roho kiuhalisia itaitwa uhai unaopita katika viungo kwa maji ukitengana na mwili ,mwili hukauka na kuanguka..
Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini? [276]. (AL - ANBIYAA: 30).
Lakini hiyo roho sio kama roho ya mtu iliyonasibishwa kwa Allah kwa lengo la kutukuza na wala hafahamu yeyote uhakika wake ila Allah wala hiyo roho haimhusu yeyote zaidi ya mtu. Basi roho ya mtu ina maanisha amri ya kiungu na haitakikani kwa mtu kuufahamu uhakika wake. Nayo ina maana ya kuingia kwa nguvu ya kutikisa ndani ya mwili ikiongezeka na nguvu ya kufikiria (akili), na kupata elimu na imani na hili ndilo linaitofautisha na roho ya mnyama.