Njia ya uchinjaji katika uislamu ya kukata shingo ya mnyama kwa kisu kikali ni huruma mno kuliko njia ya kupiga shoti na kunyongwa ambayo huadhibiwa nayo mnyama, kule kukatika kwa kuruka kwa damu kutoka kwenye ubongo ukweli ni kwamba mnyama hahisi maumivu kabisa ,na kutingishika kwa nyama wakati wa kuchinjwa sio kwa sababu ya maumivu, bali ni kwa sababu ya kuchupa kwa damu na inarahisisha damu kutoka yote nje, njia nyingine kinyume na hiyo ya kuzuia damu ndani ya mwili wa mnyama ni njia itakayomdhuru mlaji wa nyama ya mnyama huyo.
Amesema Mtume swala na salamu ziwe juu yake : Hakika Allah amehukumu wema ufanyike kwa kila kitu, mkiwa mnaua uweni vizuri na mkiwa mnachinja chinjeni vizuri,na mmoja wenu anoe kisu chake na amstareheshe mnyama wake. (Amepokea Muslim) (275)