Nyama ni chanzo cha protini, na binadamu ana meno ya magego na meno chonge kwa ajili ya kuchanga na kuchana nyama. Allah amemuumbia mwanadamu meno mazuri ya kulia mimea na nyama, na akawaumbia mmeng'enyo wa chakula mzuri kwa ajili ya kumeng'enya mimea na nyama, na hili ni dalili ya uhalali wake.
Mmehalalishiwa wanyama wa mifugo....[266]. (AL-MAIDA: 1).
Na imekuja katika Qur'an tukufu baadhi ya kanuni zinazofungamana na vyakula.:
Sema: Sioni katika yale niliyo funuliwa mimi kitu kilicho harimishwa kwa mlaji kukila isipo kuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayo mwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [267]. (AL - AN-A'AM:145).
Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. [268]. (.AL - MAIDA: 3).
Allah (aliyetukuka hali yakuwa yupo juu) amesema:
kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao fanya israfu.[269] . (AL - A'RAAF: 31)
Amesema Ibnul Al-Qayyim Allah amrehemu( 270): "Akawaelekeza waje wake kuingiza mwilini kile kinachoimarisha mwili katika chakula na vinywaji, na iwe kwa kiasi kitakacho faidisha mwili katika kiwango na namna maalumu endapo akizidisha atakuwa amefanya israfu ,na mambo yote mawili ni hatari kwa afya na husababisha magonjwa mambo hayo nakusudia kutokula na kufanya israfu,kwa hiyo linda afya kwa maneno hayo mawili.
Amesema Allah akimsifia Mtume wake "(Mtume huyo)anawahalalishia vizuri na anawahalalishia vichafu"..[271]. Akasema Allah aliyetukuka na yupo juu : "wanakuuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri"[272]..(AL - MAIDA: 4).(AL - A'RAAF: 157).
Kila kizuri ni halali na kila kichafu ni haramu.
Na ameweka wazi Mtume( swala na salamu zimuendee) kile kinachomfaa muumini katika chakula chake na kinywaji chake akasema: hajapatapo mwanadamu kujaza chombo cha shari zaidi ya tumbo lake, inamtosha mwanadamu chakula kinachoweza kuusimamisha mgongo wake ikiwa hapana budi basi (agawe tumbo lake sehelu tatu) theluthi iwe kwa ajili ya chakula na theluthi kwa ajili kinywaji chake na theluthi ya kupumulia" 273 ( Amepokea : Tirmidhiy )
Amesema Mtume swala na salamu ziwe juu yake : Hakuna madhara wala kudhuriana. (274) (Amepokea Ibnu Maga)