Kitabu hiki kina lengo la kujibu maswali ya kawaida kuhusu dini ya Uislamu ili kuwafahamisha watu dini hii tukufu, na kubainisha upekee wake, ubora wake na uwezo wake wa kihistoria wa kujumuisha tamaduni na watu mbalimbali, na kubaki sambamba na matukio na kufuatilia maendeleo, pamoja na uimara wake na uwezo wake wa kudumu licha ya jaribio lenye nia mbaya la kupotosha taswira yake na ustahimilivu wake mbele ya propaganda hasi inayoelekezwa dhidi yake, ambayo inauita kwa ugaidi na kuhamasisha watu kupambana nayo.
Na mimi namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kufanya kitabu hiki kuwa kama taa inayoangaza njia mbele ya watafutaji wa ukweli na wale wenye akili na mioyo wazi, na kiwe ni ujumbe wa amani kwa wote ili kufahamu dini ya Uislamu.