Swali: 5- Taja baadhi ya neema za Mwenyezi Mungu juu yako.

Jawabu: 1- Neema ya uislamu, nakuwa wewe si katika watu wapingaji.

2- Neema ya mafundisho ya Mtume (Sunna), nakuwa wewe si miongoni mwa wazushi.

3- Neema ya uzima na afya, kama masikio na macho na kutembea na zinginezo.

4- Neema ya vyakula, vinywaji na mavazi.

Na neema zake Mtukufu juu yetu ni nyingi hazihesabiki wala hazidhibitiki kwa idadi maalumu.

Amesema Allah Mtukufu: "Na mkijaribu kuzihesabu neema za Mwenyezi Mungu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utofauti wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso". [Suratun nahli: 18]