Jawabu:
1- Ghushi, na miongoni mwake: ni Kuficha aibu za bidhaa.
Na kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alipita katika gunia la chakula, akaingiza mkono wake ndani yake, vidole vyake vikapata unyevunyevu, akasema: "Ni nini hiki ewe muuza chakula?" Akasema: Kimenyeshewa na mvua ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Kwa nini usikiweke juu ili watu wakione? Yeyote mwenye kudanganya si miongoni mwangu" Imepokelewa na Imamu Muslim
2- Riba: Na miongoni mwake, ni kuchukua deni la elfu moja kwa mtu ili nije kumlipa elfu mbili.
Na ziada ndio riba iliyoharamishwa.
Amesema Allah Mtukufu: "Na amehalalisha Mwenyezi Mungu biashara na akaharamisha riba" [Suratul Baqara: 275].
3- Udanganyifu na kutoeleweka: Kama kuuza maziwa yakiwa katika chuchu za mnyama, au kuuza samaki wakiwa majini kabla ya kuwavua.
Imekuja katika hadithi: "Alikataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake biashara ya udanganyifu" Imepokelewa na Imamu Muslim