Jawabu:
1- Wajibu (Faradhi): Mfano kama swala tano, na kufunga mwezi wa ramadhani, na kuwatendea wema wazazi wawili.
-Jambo la wajibu hulipwa thawabu mfanyaji wake ni huadhibiwa mwenye kuliacha.
2- Sunna: Mfano kama swala za sunna zenye mpangilio (Sunani Rawatibu) Na kisimamo cha usiku, na kulisha chakula, na kutoa salamu, na huitwa sunna au Mandubu.
-Jambo la Sunna hulipwa mfanyaji wake na wala haadhibiwi mwenye kuliacha.
Angalizo muhimu:
Ni lazima kwa kila muislamu anaposikia kuwa jambo hili ni sunna au linapendeza (Mandubu) afanye haraka kulitekeleza, na kumuiga Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
3- Haramu: Mfano kunywa pombe na kuwaasi wazazi wawili, na kukata udugu.
-Haramu hulipwa mwenye kuiacha na huadhibiwa mwenye kuifanya.
4- Machukizo (Makruhu): Mfano kama kupokea na kutoa au kumpa mtu kwa mkono wa kushoto, na kufunua nguo ndani ya swala.
-Machukizo hupata malipo mwenye kuyaacha na wala haadhibiwi mwenye kuyafanya.
5- Halali: Mfano kama kula tufaa (Apple) na kunywa chai, na huitwa: yanayoruhusiwa au kwa jina jingine halali.
-Mambo ya halali hapati malipo mwenye kuyaacha na wala haadhibiwi mwenye kuyafanya.