Swali: 15- Ni zipi sharti sahihi za kufanya toba?

Jawabu: 1- kujiondoa katika dhambi.

2- Kujuta kwa yaliyopita.

3- Kuazimia kutorudia kosa.

4- Kurudisha haki na mali za dhulma kwa wenye nazo.

Amesema Allah Mtukufu: "Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al Imran: 135]