1- Ni nafsi yenye kuamrisha maovu: Nako ni mtu kufuata yale ambayo nafsi yake inamtuma na matamanio yake katika kumuasi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, Amesema Mtukufu: "Hakika nafsi huamrisha maovu mno, isipokuwa ile ambayo Mola wangu mlezi aliyoirehemu, Hakika Mola wangu Mlezi ni msamehevu na Mwenye kurehemu" [Suratu Yusuf: 53] 2- Shetani: Na huyu ni adui wa mwanadamu, na lengo lake ni kumpoteza na kumtia wasi wasi ili aingie katika shari na amuingize motoni. Amesema Mtukufu: "Na wala msifuate nyayo za shetani, hakika yeye kwenu nyinyi ni adui wa wazi". [Suratul Baqara: 168]. 3- Watu waovu: Wanaohamasisha katika shari, na wanazuia kheri. Amesema Mtukufu: "Marafiki katika kumuasi Mwenyezi Mungu duniani watatengana wao kwa wao Siku ya Kiyama. Lakini wale waliofanya urafiki juu ya uchaji Mwenyezi Mungu, urafiki wao utadumu duniani na Akhera". [Suratuz zukhruf: 67]