Jawabu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, Allahu Akbaru, "Sub-haanalladhi sakh khara lanaa haadhaa wamaa kunnaa lahu muqriniina, wa inna ilaa rabbinaa lamunqalibuun" Allaahumma inna nas aluka fii safarina haadhaa albirra wattaqwaa waminal amali maa tardhwaa, Allaahumma hawwin a'lainaa safaranaa haadhaa wat-wi anna bu'dahu, Allaahumma antas swaahibu fis safari, wal khaliifatu fil ahli, Allaahumma inni audhubika min wa'thaais safari, waka aabatil mandhwari, wasuuil munqalabi fil maali wal ahli" Maana yake: Mwenyezi Mungu mkubwa, Mwenyezi Mungu mkubwa, Mwenyezi Mungu mkubwa «Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake. Na hakika sisi kwa Mola wetu ni wenye kurejea» Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na uchamungu, na katika amali zile unazoziridhia, ewe Mwenyezi Mungu turahisishie safari yetu hii na utupunguzie umbali wake, Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye rafiki katika safari, na ndiye msimamizi katika familia, Ewe Mwenyezi Mungu hakika najilinda kwako kutokana na uchovu wa safari, na mandhari mabaya, na kurejea kubaya katika mali na familia.
Na anaporejea basi atasema maneno hayo, na ataongeza neno:
"Aayibuun, taaibuun, aabiduun, lirabbinaa haamiduun" tumerejea, na tumetubia, na tunamuabudu Mwenyezi Mungu, na kwa Mola wetu ndiko tunakorejesha shukurani. Imepokelewa na Imamu Muslim