Swali: 19- Unasema nini asubuhi na jioni katika adhkari?.

Jawabu: 1- Ninasoma ayatul kursiy: (Itazame katika msahafu) "Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye hakuna yeyote anayestahiki uungu na kuabudiwa isipokuwa Yeye. Ndiye Aliye hai Ambaye Amekusanya maana yote ya uhai mkamilifu unaolingana na utukufu Wake. Ndiye Msimamizi wa kila kitu. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Kila kilichoko kwenye mbingu na kilichoko kwenye ardhi ni milki Yake. Na hatajasiri mtu yeyote kuombea mbele Yake isipokuwa kwa ruhusa Yake. Ujuzi Wake umevizunguka vitu vyote vilivyopita, vilivyoko na vitakavyo kuja. Anajua yaliyo mbele ya viumbe katika mambo ambayo yatakuja na yaliyo nyuma yao katika mambo yaliyopita. Na hakuna yeyote, katika viumbe, mwenye kuchungulia chochote katika elimu Yake isipokuwa kadiri ile ambayo Mwenyezi Mungu Amemjulisha na kumuonyesha. Kursiy Yake imeenea kwenye mbingu na ardhi. Kursiy ni mahali pa nyayo za Mola, uliyo mkubwa utukufu Wake, na hakuna ajuwaye namna ilivyo isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Wala hakumuelemei Mwenyezi Mungu Aliyetakata kuzitunza. (hizo mbingu na ardhi).Yeye Ndiye Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, kwa dhati Yake na sifa Zake, Aliyekusanya sifa za utukufu na kiburi. Aya hii ni aya tukufu zaidi katika Qur’ani, na inaitwa Āyah al- Kursīy." [Suratul Baqara: 255]. 2- Na ninasoma: Bismillaahir rahmanir rahiim. "Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo." "Mwenyezi Mungu ndiye mkusudiwa" (2) «Hakuzaa wala hakuzaliwa" «Wala hakuna yeyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.» Mara tatu. "Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake." Sema «Najilinda kwa mola wa mapambazuko". «Kutokana na shari la viumbe na udhia wao" «Na shari ya usiku wenye giza jingi uingiapo na ujikitapo na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake." «Na shari ya wachawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga." «Na shari ya hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Alizowaneemesha ziwaondokee.» Mara tatu. "Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake." "Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu" "Mfalme wa watu" (2) "Mola wa watu" «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» Mara tatu. 3- "Allaahumma anta rabii Laa ilaaha illaa anta, khalaqtanii wa ana abduka, wa anaa a'laa 'ahdika wawa'dika mastatwa'tu, audhubika min sharri maa swana'tu, abuu u laka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambii faghfirlii fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Tafsiri yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ni mja wako, hakuna Mola isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako, na mimi niko ndani ya ahadi yako, na ahadi yako (ninafanya) kadiri niwezavyo, ninajilinda kwako kutokana na shari ya yale niliyoyafanya, nina kiri kwako kwa neema zako juu yangu, na nina kiri kwako dhambi zangu, nisamehe, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila wewe". Imepokelewa na Al-Bukhaariy