Jawabu: Ni kueleza kwa namna inayoendana na uhalisia wa tukio au kukieleza kitu kama kilivyo.
Na katika namna zake:
Ukweli wakati wa mazungumzo na watu.
Ukweli katika ahadi.
Ukweli katika kila kauli na kitendo.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Hakika ukweli unamuongoza mtu katika wema, na hakika wema unamuongoza mtu katika pepo, na hakika mtu husema kweli mpaka anakuwa mkweli" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.