Jawabu:
1- Amana katika kuhifadhi haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aina zake: Amana katika utekelezaji wa ibada kama swala, zaka, swaumu, Hijja, na zinginezo katika zile alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu juu yetu.
2- Amana katika kuhifadhi haki za viumbe:
Ikiwemo kuhifadhi heshima za watu.
Na mali zao.
Na damu zao.
Na siri zao, na yote ambayo watu wamekuamini.
Amesema Mwenyezi Mungu katika kutaja sifa za waliofaulu: "Na wale ambao wanavitunza vitu vyote walivyoaminiwa navyo, na wanatekeleza ahadi zao zote." [Suratul Mu'minun: 8]