Swali: 28- Uoga ni nini? Na ushujaa ni nini?

Jawabu: Uoga: Ni mtu kuogopa kitu ambacho hakitakiwa kuogopwa.

Mfano: Kuogopa kusema ukweli na kukemea uovu.

Ushujaa: Ni kujitosa katika ukweli, nao ni kama mfano wa kwenda mbele katika viwanja vya vita kwa ajili ya kuutetea uislamu na waislamu.

Na alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema katika dua yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na uoga". Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Allah kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri" Imepokelewa na Imamu Muslim