Swali: 27- Nini maana ya ubadhirifu? (ufujaji) Na nini maana ubahili? Na ukarimu ni nini?

Jawabu: Ubadhirifu: Ni kutumia mali bila sababu za msingi.

Na kinyume chake: Ni Ubahili: Nako ni kuzuia kutoa katika jambo la lazima.

Na sahihi zaidi nikuwa katikati ya hayo, na muislamu anatakiwa kuwa mkarimu.

Amesema Allah Mtukufu: "Na wale ambao wakitumia mali zao hawapitishi kipimo katika kutoa wala hawabani katika matumizi, na kutumia kwao huwa kuko kati na kati baina ya kupitisha kipimo na kubana." [Suratul Furqan: 67],