Jawabu: 1- Hasira nzuri: Nayo ni ile inayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pale makafiri au wanafiki au wengineo wanapoyaendea maharamisho yake Mtukufu.
2- Hasira mbaya: Nayo ni hasira inayompelekea mtu kufanya au kuzungumza mambo yasiyofaa.
TIBA YA HASIRA MBAYA:
Udhu - kutawadha.
Kukaa ikiwa atakuwa kasimama, na kulala ikiwa atakuwa amekaa.
Ashikamane na usia wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hilo: "Usikasirike"
Aidhibiti nafsi kutosukumwa na hasira akafanya maamuzi mabaya.
Kujikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa
Kunyamaza.