Swali: 24- Uvivu ni nini?

Jawabu: Ni kuwa mzito katika kufanya mambo ya kheri na yale ambayo ni ya wajibu kwa mtu kuyafanya.

Na katika hayo ni kuwa mvivu katika kutekeleza majukumu.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Mwenyezi Mungu kwa Imani wanayojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichikana kwa Mwenyezi Mungu, na hali ya kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekana na kusikika. Na wao hawamtaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache". [Suratun Nisaa: 142]

Ni lazima kwa muumini kuacha uvivu, kuzubaa na kukaa, na aende mbio katika amali na achangamke na afanye bidii na juhudi katika maisha haya kwa yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.