Jawabu: Ni kumsema ndugu yako muislamu kwa yale anayoyachukia akiwa hayupo katika mazungumzo.
Alisema Allah Mtukufu: "Na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi, Je yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo (bila shaka) Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba, mwenye kurehemu" [Suratul Hujurat: 12].