Swali: 19- Elezea unyenyekevu ni nini?

Jawabu: Ni mtu kutojiona yeye ni bora kwa watu, akawa hawadharau watu na wala haikatai haki.

Amesema Allah Mtukufu: "Na waja wa Arrahman mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha" [Suratul Furqan: 63], Yaani: Wakiwa wanyenyekevu. -Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Na hajawahi kunyenyekea yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua" Imepokelewa na Imamu Muslim Na amesema Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha wahyi kwangu, yakuwa kuweni wanyenyekevu kiasi kwamba asifanye uovu mmoja wenu kwa mwingine, na asichupe mipaka mmoja wenu juu ya mwingine". Imepokelewa na Imamu Muslim