Swali: 17- Husuda ni nini?

Jawabu: Ni kutamani neema ziwaondokee wengine, au kuchukia neema walizo pewa mtu.

Amesema Mtukufu: "(Na ninaomba kinga kutokana) Na shari ya hasidi anapofanya husuda" [Suratul Falaq: 5]

Na Kutoka kwa Anasi bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: "Msichukiane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, nakuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja" Ameipokea Bukhari na Muslim.