Swali: 16- Eleza nini maana ya bashasha?

Jawabu: Ni ukunjufu wa uso, pamoja na furaha, tabasamu, upole na kudhihirisha furaha wakati wa kukutana na watu.

Nayo ni kinyume cha kukunja sura mbele za watu, kitu kinachoweza kuwafanya wakawanaye mbali.

Na katika faida zake, zimekuja hadithi nyingi, Kutoka kwa Abuu Dhari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: alisema kuniambia mimi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Usidharau kabisa katika wema kitu chochote, hata kama ni kukutana na ndugu yako kwa uso mkunjufu." Imepokelewa na Imamu Muslim Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Tabasamu lako katika uso wa ndugu yako ni sadaka" Kaipokea Imamu Tirmidhiy